Jinsi ya kupima wazo la biashara

Jinsi ya kupima wazo la biashara

Wazo la biashara ambalo hujalipima kama linakubalika ama la laweza geuka bomu la kukumalizia mtaji wako. Make sure you validate your idea.

1. Jaribu kuangalia kama kuna mwingine anaefanya biashara kama unayoiwaza.

2. Jaribu kuzungumzia wazo lako kwa watu unaowaamini wakupe mitazamo yao juu ya wazo lako.

3. Jaribu kutengeneza bidhaa chache (kama ni bidhaa) ama jaribu kuhudumia watu wachache wa karibu yako (kama ni huduma).

4. Jijengee jina la biashara yako kwa speed kubwa kabla mwingine hajakupiku.

5. Waza namna utavyowapata wateja wa awali kabla hata hujajikita kutengeneza mchanganuo mreefu ambao mara unapomaliza kuuandaa huwa unakuwa ushapitwa na wakati.

6. Kumbuka ni kazi nyepesi kuuza bidhaa inayokubalika kuliko kuwakubalisha watu bidhaa uliyoizalisha. Hivyo basi usizalishe kitu ambacho hujawa na uhakika kama kinahitajika. Tumekuwa na desturi ya kudhania kuwa kwakuwa kila siku watu wanajenga basi tukifungua duka la vifaa vya ujenzi tutatengeneza pesa. Hii ni desturi hafifu. Kabla hujafungua hilo duka angalia yaliyopo na mapungufu yake ndipo uje na suluhu ya matatizo hayo. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

1 Comment

  1. Ni kazi nyepesi kuuza bidhaa inayokubalika kuliko kuwakubalisha watu bidhaa uliyoizalisha. Hivyo basi usizalishe kitu ambacho hujawa na uhakika kama kinahitajika. Tumekuwa na desturi ya kudhania kuwa kwakuwa kila siku watu wanajenga basi tukifungua duka la vifaa vya ujenzi tutatengeneza pesa. Hii ni desturi hafifu. Kabla hujafungua hilo duka angalia yaliyopo na mapungufu yake ndipo uje na suluhu ya matatizo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*