Kanuni ya 80/20 umewahi isikia? Unaielewa?

Kanuni hii inatuambia kuwa katika kila mambo kumi tunayopanga kuyafanya lazima tuchague mawili yatayoweza kutufanya tufikie asilimia 80 ya malengo yetu.

Kanunu hii inamaana ni muhimu sana kupembua mambo yote tunayotaka kuyafanya ili tujue kwa hakika kuwa mambo gani kati ya hayo mengi tuliyoyaanisha yataweza tusaidia kutimiza asilimia 80 ya malengo yetu.

Ili uweze kuchagua mambo machache ya kuyakazania ili yakuwezeshe kufikia asilimia 80 ya malengo yako ni lazima kwanza uorodheshe mambo yote unayopaswa kuyafanya ili ufikie malengo yako.

Ukisha yaorodhesha sasa chagua yale machache kati ya yote na uyafanyie kazi. Naamini kanuni hii imeeleweka vyema. Ila sasa ntakuongezea maarifa ambayo wengi wanaoizungumzia kanuni hii wanasahau kugusia.

Kuna mambo mawili kati ya kumi madogo sana ambayo kama hutoyafanyia kazi yanaweza kukusababishia kupoteza asilimia 80 ya malengo yako.

Kwaiyo ukishachagua mambo mawili makubwa kati ya kumi yatayokuwezesha kutimiza malengo yako hatua inayofuata ni kuchagua tena mawili madogo ambayo usipoyafanyia kazi yanaweza kupelekea ukapoteza asilimia 80 ya malengo yako.

Hapa ndio watu wanapopasahau. Ndio mana unakuta mtu ana mafanikio makubwa lakini siku anakutwa na hatia labda ya kukwepa kodi anapotezwa kwenye ramani. Ama kwa wale mastaa wa marekani na ulaya anakutwa na hatia labda ya ubakaji anapotezwa kwenye ramani. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi karibu www.miamia.co.tz kujifunza zaidi.

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

1 Comment

  1. Nimefurahi Kupata Somo Ambalo Sikuwanalo Akilini Ama Nilikuwa Nalipuzia Hivyo Kupelekea Kukata Tamaa Ya Kufanya Biashara Japo Ni Ya Ujasilia Mali Mdogo

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*