Kazi kwanza kisha Mafanikio

Unakumbuka ule wimbo wa herufi A, B, C, D, E, F, G, H, I, J, K, L, M, N, O, P, Q, R, S, T, U, V, W, X, Y, Z. Hapo umeona nafasi ya herufi K ni ya 11 na M ni ya 13? K nimeichukua kuitumia kwa ajili ya neno Kazi na M nimeichukua kwa ajili ya neno Mafanikio.

Haiishii kwenye herufi tu, nilifungua kamusi ya Kiswahili na kuangalia maneno kadhaa ikiwemo Kazi na Mafanikio nikabaini neno Kazi limetangulia Mafanikio liko mbele yake.

Nilichojifunza ambacho nawe nataka ujifunze ni kwamba Kazi hutangulia Mafanikio huja mbele ya safari.

Lakini pia nilivutiwa na uwepo wa L katikati ya K na M. Nikaja na maneno matatu amabayo ni matam kuyatamka, Kazi Lete Mafanikio.

Basi huu ukawa wimbo wangu kila siku. Kazi Lete Mafanikio. Kazi Lete Mafanikio. Kazi Lete Mafanikio. Sikuwahi fikiria Mafanikio pasi na neno Kazi nyuma yake. Na naamini kwa mwendo huu mambo yatakaa sawa. Napenda Kazi sana kuliko nnavyoyapenda Mafanikio.

Kama ujuavyo ukiwa unapenda sana safari basi kuwasili uendapo ni jambo litokealo na ukipenda sana Kazi Mafanikio ni jambo litokealo. Iambie kazi yako Ewe Kazi Leta Mafanikio, nayo itayaleta.

Jambo jengine nililojifunza kabla ya herufi M kuna herufi L. Hii ina maana hufanyi tu Kazi na kupata Mafanikio papo hapo bali kuna mlango wa kuyaendea hayo Mafanikio.

Kama K ni chumba na M ni chumba basi L ndio mlango unaovitenganisha. Mlango huu umefungwa na kitasa chake hujui kilipo na ni giza. Taa yako ni maarifa na endapo utaiacha nyuma wakati wa Kazi basi kitasa cha mlango wa Mafaniki hutokiona.

Basi sote tufanye Kazi kwa Maarifa nayo Mafanikio Yatajitokeza pasi na shaka.

Kuna mfano huwa napenda kuutumia wa mfugaji kuku mmoja wa kitanzania. Yeye hununua kila kitu dukani. Chakula cha kuku anunuacho hutokana na nafaka tunayoilima kwa matumizi ya binadamu kisha huuzwa na kufika hadi nchi jirani.

Nafaka zikifika huko huzalishwa chakula cha kuku na kuja kuuzwa kwetu. Tunaambiwa tukilisha kuku wetu chakula hicho watanawiri.

Basi mfugaji yule akaazana kununua chakula. Mwisho kuku akakua na akapiga hesabu inemgarimu shilingi 5,800 kumfikisha alipo. Alipoenda sokoni anasikia bei hairidhishi akawa ananyongeka sana.

Nilichomwambia ni kitu kimoja tu kama kweli tutaendelea kushindania chakula cha aina moja kati ya binadamu na wanyama basi wanyama wetu watakuwa ghali sana.

Ifike wakati tutambue inapaswa kuwa tofauti chakula cha wanyama na chakula cha wanadamu. How can animals and human compete over same food and expect the animal to be cheaper?

Zipo nafaka zilimwazo maalum kwa ajili ya wanyama. Nafaka hizo hazihitaji jitihada kubwa na ni nafaka nafuu na hakuna binadam alie tayari kuzitumia kama chakula. Hizi ndio zinapaswa kuelekezwa kwa wanyama.

Nilibahatika kumuona Mama akifuga kuku wale waitwao wa kienyeji kwa miaka mingi. Sikuwahi muona mama akichota zile dagaa tulopaswa kula kama mboga akawapa kuku bali niliona dagaa ikiwa mboga yetu na kuku nae pia akiwa mboga yetu.

Sasa wewe unataka kuku ale samaki wetu ili nasi tumle kuku, hapana haiwi hivyo. Kama ni protin bora nitafute namna ya kufuga mende na kuwaingiza kuku wawale hao mende wapate protin mana mende si wa thamani kwangu bali kwa kuku ni wa thamani.

Hii mada ni ndefu ila hata kwa ufupi huu naamini imeeleweka. Karibu www.miamia.co.tz/swahili tupeane maarifa. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*