Kwa mwenye ndoto ya kweli ya ujasiriamali utajiri hujileta

miamiatz kukuzamaarifa kuongezaustawi

Kama una ndoto ya dhati ya ujasiriamali, utajiri kwako utajileta wenyewe. Mwenye ndoto ya ujasiriamali ni mtu tofauti na yule mwenye ndoto ya utajiri. Ujasiriamali huwa na malengo tofauti na utajiri ila utajiri hujitokeza wenyewe katika safari ya kutekeleza ndoto ya ujasiriamali.

Tunakosea wapi?

Tatizo kubwa wengi wetu tuna ndoto za utajiri badala ya kuwa na ndoto za ujasiriamali. Mwenye ndoto ya kweli ya ujasiriamali huyaona matatizo ama changamoto wanazopitia watu wanaomzunguuka na watu wote kwa ujumla. Yeye ndoto yake huwa kutatua hizo changamoto na matatizo yanayoikabili jamii.

Sasa tufanyeje?

1. Hatua ya kwanza kuwa tayari kusoma hiki na kipe nafasi katika ubongo wako. Ukiweka ukinzani usio na msingi hakitokusaidia.

2. Hatua ya pili ya kuwa na ndoto sahihi ni kufuta ndoto ya kutajirika.

3. Hatua ya tatu ni kubeba ndoto ya kijasiriamali. Hii itakusaidia kuyaona matatizo na changamoto kibao zinazoikabili jamii.

4. Hatua ya nne ni kuangalia namna ya kuyatatua matatizo na changamoto zinazoikabili jamii. Unajua sio lazima kila siku uwaze namna ya kuuza bidhaa kwa ajili ya kujipatia pesa. Jamaa wa fcbk, Mark alipoanzisha fcbk lengo ilikuwa ni kutengeneza kijiwe mtandaoni ambacho watu wanaweza kupiga stori na kujadili mambo bila hata kuwa ana kwa ana.

5. Usiweke lawama kubwa kwenye mfumo wa elimu kama kisingizio cha umaskini wako wa fikra na fedha. Kupambania maisha ni vita yako na kama umepewa zana butu za mapambano zitupe kule chonga zana zako.

Mifano ya walioona elimu za ughaibuni ni zana butu wakachonga zana zao na wakafaulu mapambano yao ni kama:

1. Billgates tajiri wa matajiri bilionea wa mabilionea mmiliki wa microsoft.

2. Mark Zuckerburg bilionea mmiliki wa facebook, whatsapp, instagram etc.

3. Steve Jobs marehemu mmiliki wa Apple. Japo sijawahi miliki macbook wala iphone ila namkubali sana huyu jamaa💪👏👏👏.

4. Oprah. Mama bilionea anaejiamini na kupendwa na wengi weupe kwa weusi.

5. Abraham Lincolin aliekuwa raisi wa lile linchi likubwa libabe (marekani).

6. Walt Disney marehemu yule mwenye channel kibao kwenye dstv za vikatuni katuni na michezo ya watoto.

7. Brad Pitt. Tajiri katika tasnia ya muvi. Jamaa wa war machine, furry, allied etc kwa wapenzi wa muvi mnazijui hizi kitu.

8. Acha nisikuchoshe mana list ni ndefu sana. Wapo wengi.

Kwaiyo msidhani kuwa mfumo wa elimu ni mbaya tu bongo, hata ughaibuni kuna shida japo zinazidiana.

Tujifunze kuyaona matatizo ya jamii – Tubuni namna ya kuyatatua.

Kawaida watu watakuwa tayari kutumia pesa pale ambapo wanaona suluhu ya matatizo yao. Ona wachina waliona kuwa tatizo la wadada wa bongo wanapenda shepu wakaleta madawa ya kuongeza shepu.

Uber waliona adha ya usafiri wa bongo wakaleta mfumo wa taxi ulioboreshwa.

Hata mtaani kuna matatizo na sote tunapaswa kutafuta suluhu ya matayizo ndio hapo iwe chanzo cha kupata kipato.

Kwangu mimi mjasiriamali ni mtu anaeyaona matatizo ya wengine na kuyatafutia suluhu na kuwatoza malipo kulipia suluhu hiyo. Kumbuka www.miamia.co.tz ndio nyumbani kwetu MIAMIA. Tunakaribisha wageni wote watutembelee. Nawasilisha. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*