Mfumo wa BRELA wa kusajili biashara mtandaoni

Fursa ya biashara ya kilimo cha nyonyo

Mfumo wa usajili wa biashara mtandaoni (OBRS) ni mfumo wa kimtandao ambao BRELA waliuanzisha kwa malengo ya kuwawezesha watanzania popote wawapo kuweza kusajili majina ya biashara zao kwa kutumia mfumo wa computer, simu za mkononi, na tablet zilizounganishwa mtandaoni. Mfumo huu umeondoa haja ya mtu kutembelea ofisi za BRELA zilizopo Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya usajili wa majina ya biashara.

Unachoweza kufanya kupitia mfumo huu wa OBRS

=> Kutafuta na kuona kama jina la biashara ama kampuni laweza sajiliwa,
=> Kusajili jina la biashara na kupata vyeti vya usajili mtandaoni,
=> Kuomba kutunziwa jina la biashara ama kampuni kwa kipindi flani kabla hujasajili,
=> Kuangalia taarifa mbalimbali zilizosajiliwa katika kumbukumbu za BRELA,
=> Kubadili taarifa za biashara.

Namna mfumo huu unavyofanya kazi

Jisajili kwenye mfumo huu wa OBRS kwa kufungua https://ors.brela.go.tz

Ili uweze kujisajili katika mfumo wa OBRS unapaswa kuwa na vitu vifuatavyo:

=> Anuani ya barua pepe,
=> Namba ya simu,
=> Kitambulisho (Kadi ya mpiga kura, Kitambulisho cha utaifa, Pasi ya kusafiria, ama Leseni ya udereva).

Ukishajisajili, mfumo wa OBRS utakutumia barua pepe kwenye anuani yako ya barua pepe na pia utapokea ujumbe mfupi kwenye simu yako kukujulisha kuwa umefankiwa kujisajili.

Kinachofata ni wewe kuingia katika mfumo wa OBRS na huko utaweza kufanya yafuatayo:

=> Kuangalia kama jina la biashara linaweza kusajiliwa,
=> Kuangalia kama jina la kampuni linaweza kusajiliwa.

Ndani ya muda mfupi utajulishwa na mfumo huo kuwa jina uliloomba linaweza kusajiliwa ama la. Endapo umejulishwa kuwa jina la biashara linaweza kusajiliwa basi utapaswa kufanya malipo kama utavyoelekezwa kwenye huo mfumo wa OBRS na baada ya malipo jina la biashara litasajiliwa.

Malipo yanaweza kufanyika kwa:

=> Kuweka pesa benki ya CRDB kupitia Cash deposit, Sim Banking, Fahari Huduma ama Internet Banking,
=> Kutuma pesa kwa MPESA/TigoPesa/Airtel Money;
=> Kuweka pesa benki ya NMB kupitia NMB Mobile.

{module General Adsense Ad}

Ili kusajili jina la biashara unapaswa kuweka taarifa zako kama ifuatavyo:
=> Taarifa za ujumla za biashara (anuani ya barua pepe, anuani ya posta, namba ya simu, unaweza kutumia taarifa zako kama huna zile za biashara yako)

Baada ya kukamilisha usajili, utaweza kuprinti vyeti vyako vya usajili ambavyo vitatumika kwa siku 30 na baada ya hapo utapaswa kuwa na vyeti halisi ambavyo BRELA watakutumia kwa anuani ya posta.

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

7 Comments

  1. Naitaji kusajiri bihashara yangu ya stationary Kwa jina la Kyeshe general supplis

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*