Mtaji wa pesa huna je na mtaji wa nguvu huna?

Nguvu iwe za akili na za mwili pia ni mtaji. Ukizitumia vyema nguvu hizo na ukidhibiti vyema matumizi yako utaweza kutoboa tu. Kuna watu wapo tayari kukulipa kiasi flani cha pesa kwa kuwasaidia kazi flani.

Bahati mbaya sana watu hawawezi kuziona nguvu zako za kimwili wala kiakili kwa kukutazama haiba yako. Ni sharti uidhihirishe ndipo uweze wafanya watu waanze kukupa kazi.

Hata mcheza mpira haajiriwi kabla hajadhihirisha kipaji chake iweje wewe unataka watu wakupe kazi kwa kuwaonesha haiba, maumbile na makaratasi?

Dhihirisha kipaji chako watu watakuona na watakufungulia fursa. Katika kudhihirisha kipaji lazima uwe na uvumilivu mana huwa inachukua muda mrefu kabla kipaji chako hakijaonekana.

Na kikionekana usibweteke. Wapo waliodhihirisha vipaji vyao wakapewa fursa wakabweteka na kuvimba vichwa wakafulia. Usije nawe ukaangukia katika dhahama hii.

Kwa wale waliobarikiwa wakapata elimu basi watafute hata kazi za kujitolea. Na usiyaamini makaratasi kuwa yatakupatia kazi hata hiyo ya kujitolea. Kama kweli umeamua kujitolea basi hebu jitolee ufanye kazi na ukienda ofisi za hao unaotaka wakupe kazi uwasilishe kazi yako.

Mathalan fani yako ni masuala ya masoko, basi fanya uchunguzi sokoni uone hao unaotaka wakupe kazi wanakabiliwa na changamoto gani ambazo zikitatuliwa itapelekea bidhaa zao zitauzika zaidi? Karibu www.miamia.co.tz/swahili ujifunze zaidi. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*