Elimu ni muhimu sana katika ujasiriamali

Kuna mahali nilipita kula chakula cha jioni. Ilikuwa majira ya sambili kasoro usiku. Huwa sipendi kula zaidi ya samoja jioni ila ilinibidi nile kwa sababu nilikuwa na njaa na sikuwahi kula.

Nikaagiza chakula na chai ya maziwa. Cha ajabu nilikutana na chai imejazwa iliki na pilipili manga kibao. Nilishangaa kidogo nikapata wazo la kundika makala hii.

Unapoamua kujiingiza katika biashara flani jaribu kutafuta maarifa kuhusu biashara hiyo. Unajiskiaje ukiingia duka la dawa ukahudumiwa na mtu anaeijua dawa unayotaka kununua kwa kina na akaweza kukushauri zaidi? Bila shaka utajiskia nafuu hata kabla hujaitumia hiyo dawa.

Hivyo basi unapojiingiza katika biashara flani hebu jaribu kujua mambo nyeti ya biashara hiyo. Mwenye mgahawa niliokula angekuwa anajua aina ya vyakula mtu anatakiwa ale muda gani angeandaa menu nzuri na hata kuweka vipeperushi mezani juu ya ulaji bora.

Badala yake yeye mwenyewe tena alikuwa ndio meneja alikuwa hajui haya mambo. Usiku haishauriwi kula vyakula vyenye viungo vikali mana inapelekea tindikali kuzalishwa kwa wingi tumboni hivyo kusababisha kitu wazungu wanaita reflux.

Reflux huanza kama kiungulia kwa baadhi ya watu ila baadae huleta hali ya kukereketa kooni na mwishowe kupata michubuko makoromeoni. Michubuko huletwa na tindikali iliyozidi unapolala inakuwa inalazimika kurudi kooni.

Sasa huyu mhudumu na meneja wake ambae ndio mmiliki natamani wangelijua hili. Wangeweka menu zinazoendana na wakati. Wangeongeza pia huduma ya kuwaelekeza watu muda wajapo wanafaa wale chakula gani.

Huduma ya mgahawa lazima iambatane na ujuzi wa vyakula. Sio unapika tu ilimradi. Mi nashauri uwe unatembelea ukurasa wa www.miamia.co.tz/swahili ili ujifunze zaidi na zaidi kila siku uweze kuboresha huduma katika biashara yako ama ujipange vyema katika biashara unayoenda kuifanya.

Ukiamua kufungua hardware ukauza vifaa vya ujenzi itapendeza ukajua mambo kadhaa ya vifaa uuzavyo. Na kadhalika kwa biashara nyengine. Inapendeza ukipita duka la vifaa vya ujenzi ukaagiza balbu za nyumbani kwako mtu akakupa ushauri balbu gani inafaa kwa matumizi gani ili usije jikuta unaweka balbu sebleni panakuwa mwanga mkali kama ukumbi wa kurekodia muvi. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*