Jifunze kusema samahani kwa mteja wako

Hata kama binadamu tumeumbwa na udhaifu wa kutoyaona makosa yetu mteja wako anapolalamika kukosewa usipende kuanza ligi ya kutafuta ukweli kwamba umemkosea ama la badala yake tanguliza kuomba msamaha mana unachokiona wewe ni sahihi chaweza kuwa kwake si sahihi.

Kumbuka haitoshi tu kutamka samahani bali unapatwa kuona kuwa kweli umekosea. Mteja anapokueleza malalamiko yake usitie pamba masikio na kumuona ni mlalamikaji tu badala yake msikilize kwa umakini mkubwa mpaka uelewe anachokilalamikia.

Baada ya kuelewa jishushe na umwambie kiasi gani unajiskia vibaya kwa wewe kumkwaza. Ahidi kutojirudia kwa kile kilichotokea.

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*