La kujifunza kutoka brand kubwa

La kujifunza kutoka brand kubwa

Kwa Wanaofikiria Kuanzisha Brand zao Kuna la Kujifunza Kutoka katika Brand za Nguo Mashuhuri Duniani. Kuna brand nyingi sana za nguo duniani. Nimeona niziorodheshe 20 tu ambazo zina umaarufu mkubwa zaidi kwa sasa. Hebu pitia orodha hii kisha weka pembeni simu na ujaribu kukumbuka yoyote ambayo imekaa kichwani mwako. Hapa utaelewa umuhimu wa kuwa na brand name jepesi na pekee.

01. POLO | Ralph Lauren
02. Hugo Boss
03. Nike
04. Tommy Hilfiger
05. Levi’s
06. Burberry
07. Gucci
08. Adidas
09. Lacoste
10. Rolex
11. Versace
12. Diesel
13. Prada
14. Calvin klein
15. Armani
16. Zara
17. J. Crew
18. American Eagle Outfitter
19. Abercrombie & Fitch
20. H & M

Tuchukulie mfano upo kwenye maonyesho ya nguo na kwakuwa wabunifu wengi nguo zao zina mfanano je unadhani brand ngapi kati ya hizi zote utazikumbuka siku ya pili na ngapi utazikumbuka wiki moja baada na ngapi utazikumbuka baada ya mwezi na ngapi utazikumbuka baada ya mwaka.

Hapa kuna mambo mawili muhimu. Moja urahisi wa kulizingatia jina na la pili umaarufu wake. Jina laweza kuwa jepesi na lisiwe maarufu na jengine likawa gumu ila maarufu. Ila kama haya majina ingekuwa yote hayana umaarufu hebu fikiria lipi lingepata nafasi ya haraka ya kukaa kwenye kumbukumbu zako.

Hebu fikiri kama wewe ni mwalimu halafu darasa lina hao wanafunzi. Umeanza kufundisha darasa jipya. Kukiwa na wanafunzi wawili vichwa sana na wawili watukutu sana. Wale vichwa mmoja awe na jina jepesi sana na mwingine awe na jina gumu sana. Na wale watukutu mmoja awe na jina jepesi sana na mwingine awe na jina gumu sana.

Ukipewa nafasi ya kuorodhesha wanafunzi watano wakorofi na watano vichwa yale majina mepesi kuyashika na kuyakumbuka yatajitokeza mwanzo katika kumbukumbu zako.

Sasa katika kujenga brand hii ndio hali ilivyo. Kama brand mbili zikiwa zote mpya na wamiliki wake wakatumia njia zinazofanana kuwasilisha bidhaa zao sokoni bila mmoja kuzidi kutimia pesa nyingi kujenga umaarufu na wote wakiwa na bidhaa zenye ubora unaoendana basi jina rahisi litadumu kwenye kumbukumbu za wateja wengi kuliko jina gumu la brand. Nimeileta hii kutoa msisitizo. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*