Panga mipango ya kukuza biashara yako

Panga mipango ya kukuza biashara yako

Sio sawa wala sio haki kuwa na biashara miaka nenda miaka rudi bila kuona ukuaji wake. Wakati unaanza biashara angalia kwa kina kama biashara yako itakuwa yenye ukubwa gani miaka kadhaa ijayo. Huwa napenda kuwaambia watu kuwa na biashara ambayo huna mipango ya ukuaji wake ni sawa na kuwa na mtoto asiekuwa.

Ili uwe na biashara yenye fursa za ukuaji lazima wakati unachagua biashara yako uangalie fursa endelevu. Mfano kwa kipindi hiki cha ukuaji wa kiuchumi biashara za vyakula zinashika hatamu kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaokula migahawani. Sasa utakuta mtu kaanza kama mama ntilie ila miaka inasonga huoni ukuaji wa biashara yake ya chakula.

Hata Bakhresa alianza na mgahawa ila aliikuza biashara yake ya chakula mpaka leo hii amekuwa na viwanda vya juisi, maziwa, unga na kadhalika. Hebu tafakari, yeye aliona ananunua ngano na nafaka nyenginezo kwa wingi kulisha watu kwenye mgahawa wake. Pia aliona kuwa watu wanakunywa vinywaji vingi mgahawani kwake. Akatafakari na kuona kuna haja ya kuanza kupaki maji, juisi na kusindika mahindi na ngano. Aliiona pia hali ya hewa watu wanapenda vitu baridi akaamua kuzalisha ice cream.

Mpaka leo hii bado biashara yake inakuwa baada ya kupenya nchi kadhaa za afrika mashariki na kati. Hebu nawewe kwenye biashara uliyonayo ama unayotaka kuanzisha jaribu kutafakari kwa kina miaka 10 ijayo na miaka 20 ijayo na 30 ijayo na kadhalika itakuwa katika hali gani.

Katika hali ya masoko ya sasa mbinu za kukuza biashara ni tofauti na zile za kale. Kwa sasa kitu muhimu sana ni kujenga brand kwa speed kubwa kadiri iwezekanavyo. Wapo wanaodhani kujenga brand ni kwa kuweka matangazo kila kona. Ni kweli matangazo yanasaidia ila njia bora zaidi ni kujikita kuweka physical evidence ya ubora wa huduma ama bidhaa yako katika matangazo yako badala ya kujikita kuwaambia watu wanunue.

Utakuta kampuni flani ipo busy kurusha matangazo ya huduma ama bidhaa flani. Katika matangazo utaona mapicha picha ya bidhaa na maelezo ya wapi zinapatikana. Hii approach imepitwa na wakati. Hivi sasa watu wanapenda physical evidence na ndio maana utaona mtu kama Dk. Mwaka wa tiba asilia alijizolea umaarufu na ukuaji wa haraka wa biashara yake mana yeye hakuwa akisema tu njoo tukuhudumie bali aliueleza ugonjwa kwa kina mpaka hata aieenda shule alielewa ugonjwa anaouzungumzia ni ugonjwa gani, unasababishwa na nini na namna ya kuutibu ama kuudhibiti.

Hii ilikuwa ni evidence tosha kuwa jamaa anajua anachokizungumzia. Nimewahi ona wajasiriamali kadhaa wanaojihusisha na kuelimisha kilimo bora. Ila bahati mbaya elimu yao haina physical evidence. Wanashindwa kudemonstrate kwa kina ujuzi wao.

Physical evidence ni ule uthibitisho unaoutoa mbele za watu kuwa una ujuzi wa kutosha juu ya lile ulisemalo. Sasa unakuta mdada ana saluni na anasema wanatengeneza nywele vizuri huku yeye mwenyewe nywele zake za hovyo. Anadai ana uwezo wa kuondoa makunyanzi na kutibu wale waloungua na vipodozi na kuondoa rashes usoni na kadhalika na kadhalika afu unakuta anatumia wafanyakazi wake wenyenwe wamejaa rashes usoni na ngozi za sura zao hazieleweki kama ni nyuso ama ni ngozi za magoti zimehamishiwa usoni. Hii inakupotezea wateja wengi sana mana kuna wateja wanajua kutafakari uyasemayo na kujua kama unajitambua ama la.

Kabla hujanishawishi ninunue bidhaa ama huduma yako hebu jaribu kunithibitishia kuwa itanifaa. Sio jamaa anakuja kunambia anatengeneza website nzuri afu yeye mwenyewe hana ama aliyonayo ya ajabu ajabu. Utawapata baadhi ya wateja ila wengi utawakosa. #MiaMiatz
#KukuzaMaarifa
#KuongezaUstawi

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*