Soko linaposinyaa na bidhaa kuongezeka bei hushuka

Katika pirikapirika za biashara ni vyema kutambua kuwa kwa hali ya sasa ya kusinyaa kwa kipato na soko la bidhaa na huduma mbalimbali kunaweza pelekea bei za baadhi ya bidhaa na huduma kushuka.

Kushuka kwa bei hutokana na kanuni isemayo kuwa kadri bidhaa inavyoongezeka sokoni na wakati soko likisinyaa basi bei za bidhaa husika zitashuka.

Mathalan unaweza kuta kuwa umeongeka ufugaji wa kuku na asilimia kubwa ya wateja wako vipato vyao vinaporomoka kitakachotokea ni wateja kuomba punguzo kila kukicha.

Kama garama zako za ufugaji zinapanda basi ujue biashara hii itakuwa ni yenye hasara.

Jambo muhimu la kufanya ni kujitahidi kipindi cha ukata kujaribu kutafuta njia za ufugaji ambazo zina garama nafuu vinginevyo unaweza jikuta na mtaji unakata.

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*