Umeshasogeza bidhaa ama huduma karibu na wateja?

Katika kipindi hiki cha ukata ni muhimu sana kuisogeza bidhaa ama huduma yako jirani zaidi na wateja. Ukaribu wa bidhaa ama huduma kwa mteja hupimwa kwa kupima umbali anaotembea mteja kuifikia bidhaa ama huduma hiyo.

Huu ni ukaribu halisia wa bidhaa ama huduma kutoka alipo mteja. Ila upo pia ukaribu wa bidhaa ama huduma ambao ni ukaribu wa kihisia.

Ukaribu wa kihisia hupimwa kwa wepesi ama urahisi wa mteja kutumia bidhaa ama huduma yako. Kwa kawaida mteja anaweza kwenda mbali kufuata bidhaa ama huduma flani kama anahisi kuwa iliyopo karibu ni ngumu kuitumia.

Pia kuna wakati mteja anaweza kwenda mbali kwa kudhani tu kuwa bidhaa ama huduma iliyopo karibu nae ni kama ya watu wenye hadhi flani ambayo yeye hana hadhi hiyo.

Hapo zamani za kale kuna watu walikuwa na hisia kuwa suala la kuweka pesa benki ni la wenye pesa nyingi na matajiri. Ila mabenki wakaanza kujenga mawakala wa mabenki mathalan fahari huduma etc.

Pia mabenki wakasogeza huduma za kibenki kwenye mifumo ya simu za kiganjani. (…itaendelea…)

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*