Umuhimu wa kujifunza kujenga na kusimamia brand

Umuhimu wa kujifunza kujenga na kusimamia brand

Mimi sikuwa najua mpaka ilipofika November mwaka jana (yaani 2016). Nilipojua umuhimu wa hili jambo nikaanza kujifunza. Nilijifunza kwa nguvu zote mpaka March 2017 nikahitimu. Wakati najifunza wapo watu kadhaa ambao nilishawaandalia brand strategy na wakaifuata leo hii wao na huduma zao ni maarufu kuliko mimi. Nilikuja kustuka mwezi March 2017 baada ya kuona video ya mmoja kati ya wale niliowaandalia brand strategy akihojiwa na DW Swahili na BBC Swahili akielezea biashara yake.

Nikasema duh kumbe ameni overtake. Nami kuanzia March 2017 nikaamua kuanza kujenga jina la MiaMia nalo liwe miongoni mwa brand mashuhuri Tanzania. Kumbuka kuwa hili jina limesajiliwa kwaiyo nna haki za kisheria kulitumia na anaenakili nna haki ya kumpeleka mahakamani.

Kabla sijaanza kutumia maarifa ya brand management nilikuwa na wafuasi 603 hapo March 2017. Baada ya kuanza kuyatumia maarifa hayo basi wafuasi wakaanza kuongezeka mpaka leo hii ni karibia 30,000. Kila siku nimejipatia wastani wa wafuasi 125. Angalia picha kujionea graph ilivyoenda.

Sasa hebu fikiri kama ningekuwa ni mmiliki wa chuo nikawa napata asilimia 10 tu ya wafuasi wangu kama wanafunzi ina maana ningekuwa na wanafunzi 3,000.

Brand management inaweza tumiwa na biashara yoyote ile na ndio mbinu inayotumiwa na watu maarufu wote duniani kujizolea umaarufu. Hii mbinu ukiijua hata kama unaendesha bodaboda basi kwa siku unaweza jikuta unapakia mara mbili zaidi ya abiria uliokuwa ukipakia.

Kama kweli unaipenda biashara yako wekeza kujifunza brand management. Kwanza ukishajifunza hii kitu unaweza shangaa ukabadili msimamo na kuamua kujikita kwenye biashara tofauti kabisa ambayo itaenda speed unayotaka na kukupatia kipato kizuri zaidi.

Ubaya ni kwamba wengi wetu tunatafutaga mitaji ya kuanzia biashara ila hatutengi hata kumi ya kujifunza brand management. Ndio mana watanzania wanakuja na brand zao za nguo, manukato, vipodozi, mabegi, na kadhalika. Ila je ni kwanini hayawi maarufu kama adidas na brand zingine zinazotamba duniani? Shida kubwa ni kutojua namna ya kujenga na kukuza brand. Ila polepole tutafika tu ilimradi tuwe tayari kubadili mindset zetu. Acha miamia iendelee kutoa darasa japo wigo bado sio mpana. Kumbuka tunapatikana pia kupitia www.miamia.co.tz #MiaMiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*