Unatokaje katika madeni?

Kujitoa katika madeni ni kazi ngumu sana. Ila kama kweli unataka mafanikio ya kweli jitoe kabisa katika madeni. Kwanini nasema jitoe katika madeni? Asilimia kubwa ya wanaodaiwa wanadaiwa pesa ambazo hazizalishi chochote. Haya ni madeni bomu. Yakikulipukia yatakumaliza.

Kujitoa katika madeni kunahitaji nidhamu ha matumizi. Kila unapotaka kutumia pesa hebu jiulize je usipoitumia kwani utapata madhara makubwa kiasi gani? Kama hakuna madhara makubwa yasiyotatulika basi acha kutumia.

Ukienda kwa style hii utashangaa kuna kipindi unabakiwa na pesa za kutosha na unaepuka madeni kabisa. Bahayi mbaya ukishaanza kuwa na pesa zaidi ushawishi wa kutumia huongezeka. Hapa ni lazima ujiondoe katika baadhi ya mifumo ya maisha ambayo inakufanya utumie pesa bila mpangilio.

Halafu usiseme utaanza kesho mwezi ujao wala baadae wala mwakani. Baadae huwa haifiki hivyo anza sana. Kumbuka usitumie pesa kabla hujajiuliza hivi nisipotumia hii pesa kwani nini kinanitokea? Ntakufa? Ntateseka? Ntaweza kuvumilia mateso? Mada ngumu ila ndo muhimu. Ukitembelea www.miamia.co.tz/swahili utapata mada nyingi zaidi. Kila la heri katika safari yako ya kujitoa katika madeni. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi.

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*