Jaribu kuibadili biashara inayowatia hasara wengine kwako ikupe faida

Kwa mfano umekuta watu wamezoea kufuga kuku wa nyama a.k.a broilers na bei sokoni haziridhishi hapo ni lazima kupatikane ubunifu wa kuweza kuzalisha kuku kwa gharama za chini.

Sehemu kubwa inayoumiza vichwa kwa wafugaji ni kupanda kwa bei za vyakula vya kuku. Nilieleza kidogo katika makala iliyopita suala la wanyama na wanadamu kugombea nafaka na protini na madhara yake.

Kwa kawaida chakula chenye grade ya kuliwa na binadam huwa na garama ya juu. Chakula hicho hakikupaswa ndio kiwe malighafi ya kuzalisha chakula cha wanyama.

Ukifuga n’gombe wa maziwa akawa anakula majani ya kununua, maji ya kununua, na kila kitu cha kununua basi hapo unafanya biashara ambayo mafanikio yake ni ya kusuasua.

Kumbuka biashara kabla hujaiendea ni muhimu kupembua key success factors. Key success factors ninini? Hivi ni vigezo maalum vinavyohitajika ili kufanikiwa katika biashara flani ama katika jambo flani.

Kwa mfugaji kuku wa nyama wa kisasa key success factor namba moja ni low cost. Yaani kuweza kumudu kuzalisha kwa gharama ya chini kuliko wengine.

Nimegusia mara nyingi suala la fursa. Fursa kwako yaweza isiwe fursa kwangu kwa sababu key success factors za fursa hiyo mimi kama sina wewe unazo basi mi nikijiingiza biashara itaniangusha tu.

Mfano mtu ana shamba heka moja na analima mahindi yale ambayo hayana hadhi ya kuliwa na binadam na anatumia nafaka hiyo na majani pamoja na mabua yapatikanayo kulisha mifugo yake. Wewe ambae huna hata kipande cha ardhi kwako ufugaji utakuwa ghali kuliko yeye.

Kwakua key success factor ya ufugaji ni gharama nafuu yeye atafanikiwa haraka nawewe utasuasua.

Ili kushusha gharama za ufugaji kwanza lazima uamue kuwa wa tofauti hata kama watu wengine watakucheka ama kukuona wa ajabu.

Anza na kuku wachache na ujaribu mabaki ya vyakula na mabaki yapatikanayo baada ya kusindika matunda na mboga. Najua hofu itakua kwenye muda wa kuwaandaa mpaka wafikie uzito wa kuuzika. Ila hata sasa kuna tafiti nyingi zinaendelea duniani kuhusu matumizi ya mabaki ya vyakula na mabaki ya kusindika matunda viwandani kwa kuku.

Matokeo ya awali ya tafiti hizo yanavutia. Sasa nawe anza na kuku wachache fanyia majaribio. Kumbuka hata china hawakupata suluhisho la haraka kuhusu jambo la gharama. Walikuwa wabunifu na wakafaulu kupata low cost model katika kila bidhaa. Na kwasasa mauzo yao ni makubwa sana kiasi kwamba makampuni mengi tuliyozoea yalikiwa Ulaya sasa yamehamia ama kufungua viwanda vikubwa zaidi china.

Hii mada ni ndefu ila ntaikatisha kwa kukwambia katika kila biashara uifanyayo pembua key success factors ni zipi na je utaweza kuzifikia? Ila moja wapo katika biashara yoyote ni kuwa na gharama za chini za uzalishaji wa bidhaa. Ukikwama tupigie 0713 032 336 ama tembelea www.miamia.co.tz/swahili na utwambie unafanya biashara gani tutakwambia key success factors ni zipi. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi

About Juma Kessy 49 Articles
Napenda sana ujasiriamali. Napenda vijana wote wajue kanuni muhimu za ujasiriamali. Msingi unaoniongoza ni maarifa kwa wote. Na lengo langu kuu ni Kukuza Maarifa na Kuongeza Ustawi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*