Jinsi ya kusajili kampuni Tanzania – hatua kwa hatua

Zijue hatua 15 za kusajili kampuni Tanzania

Makala hii inaelezea hatua 15 za kusajili kampuni Tanzania. Hatua hizi zaweza ongezeka iwapo sekta husika inasimamiwa na sheria ya ziada.

Sekta zinazosimamiwa na sheria za ziada ni kama vile utalii, afya, elimu, uvuvi, nishati, madini, mafuta, gesi, na kadhalika.

Zingatia:

  1. Kampuni ni muunganiko wa watu wawili ama zaidi. Huwezi fungua kampuni peke yako kwa sheria za Tanzania.
  2. Kampuni ni taasisi binafsi inayosimama yenyewe kama yenyewe kisheria.
  3. Kampuni inaweza kushitakiwa ama kumshataki mtu ama watu ama taasisi nyengine.
  4. Wanaoendesha kampuni huitwa wakurugenzi.

Kwa wale wanaojiuliza Kampuni inatofauti na Jina la biashara? Jibu ni kwamba Kampuni ni taasisi wakati Jina la biashara ni biashara binafsi iliyorasimishwa kwa kupewa jina. Kampuni inaweza kumiliki jina la biashara. Mtu binafsi anaweza kumiliki jina la biashara. Wabia wanaweza kumiliki jina la biashara.

Estimated Cost : 750,000 – 3,400,000 TZS

Time Needed : 30 days

Hatua kwa hatua jinsi ya kusajili kampuni Tanzania.

  1. Hatua ya 1. Kusanya taarifa za wahusika

    Wahusika ni (1) wanahisa (yaani wamiliki), (2) wakurugenzi (mkurugenzi ni muendesha kampuni ambao wanaweza kuwa wanamiliki hisa ama la kwenye kampuni hiyo), (3) katibu.Kusanya taarifa za wahusika

  2. Hatua ya 2. Andaa nyaraka za usajili

    Nyaraka hizo ni Memorandum of Association, Articles of Association (Memarts) na Declarartion of Compliance (Form 14b).

    Memarts lazima isainiwe na subscribers ambao ndio waasisi wa kampuni. Memarts na form 14b lazima ziwe na muhuri wa mwanasheria.
    Andaa nyaraka za usajili

  3. Hatua ya 3. Jaza maombi kwenye BRELA ORS

    Jaza kwenye mtandao wa ors.brela.go.tz taarifa zote ulizokusanya hatua ya kwanza kwa mtiririko uliowekwa kwenye mfumo huo wa BRELA ORS.

    Bonyeza hapa kufungua makala inayoeleza jinsi ya kujaza taarifa za kampuni kwenye mfumo wa brela wa usajili wa makampuni mtandaoni.
    Jaza maombi kwenye brela ors

  4. Hatua ya 4. Download nyaraka toka BRELA ORS

    Baada ya kujaza maombi utaweza ku download consolidated form na integrity form. Ukisha download print kisha msaini kila pale panapohitaji saini. Weka tarehe kila panapohitaji kuweka tarehe.
    Download nyaraka toka brela ors

  5. Hatua ya 5. Upload nyaraka kwenye BRELA ORS

    Nyaraka hizo ni zile ulizoandaa kwenye hatua ya 2 na zile ulizodownload kwenye hatua ya 4. Scan nyaraka hizo kisha upload kwenye BRELA ORS.
    Upload nyaraka kwenye brela ors

  6. Hatua ya 6. Lipia maombi BRELA

    Ukisha upload nyaraka zote na kuendeleza maombi hayo utapatiwa bili yenye control number ambayo utapaswa kuilipia. Ukishalipia maombi yataenda BRELA kwa dhumuni la kufanyiwa kazi.
    Lipia maombi brela

  7. Hatua ya 7. Subiri maombi yafanyiwe kazi

    Maombi yatafanyiwa kazi na utapokea ujumbe kwa njia ya email ukikueleza kuwa maombi yamepitishwa na cheti kipo tayari kupakuliwa.

    Iwapo kuna marekebisho ya kufanya basi utapokea ujumbe usemao urekebishe kitu gani. Utapaswa kurekebisha na kuyatuma tena maombi na kusubiria majibu.
    Subiri maombi yafanyiwe kazi

  8. Hatua ya 8. Pakua cheti toka BRELA ORS

    Cheti kikiwa tayari utapokea ujumbe usemao kuwa cheti chako kipo tayari. Utapaswa kuingia kwenye mfumo wa BRELA ORS na kupakua cheti hicho.
    Pakua cheti toka brela ors

  9. Hatua ya 9. Omba TIN

    Utapaswa kujaza maombi ya TIN ya kampuni kwa kutumia fomu ya kuombea TIN ya kampuni.

    Utaambatanisha nakala ya Memarts, Cheti cha BRELA, utambulisho toka serekali za mitaa na mkataba wa mahali ulipopanga kwa ajili ya kufanyia shughuli za kampuni.

    Fomu na viambata vyote utapeleka ofisi za TRA zilizo karibu nawe. Unapaswa kuambatanisha pia fomu za ku update taarifa za TIN za wakurugenzi wote wenye TIN.

    Utaambatanisha pia vitambulisho vyao vya NIDA endapo hawana basi vitambulisho vya aina nyengine yoyote.
    Omba TIN

  10. Hatua ya 10. Omba leseni

    Leseni “Fungu A” huombwa wizara ya viwanda na biashara kupitia BRELA. Maombi haya hufanyika mtandaoni.

    Leseni “Fungu B” huombwa halmashauri iliyo karibu nawe (wilaya ama manispaa ama jiji).
    Omba leseni

  11. Hatua ya 11. Sajili NSSF

    Nenda kasajili kampuni NSSF. Utapaswa kufika kwenye ofisi za NSSF zilizo karibu na ofisi ya kampuni yenu.
    Sajili NSSF

  12. Hatua ya 12. Sajili OSHA

    Usajili wa OSHA huweza kufanyika mtandaoni. Ingia kwenye tovuti ya OSHA kufanya maombi ya usajili.
    Sajili OSHA

  13. Hatua ya 13. Sajili WCF

    Maombi ya usajili WCF hufanyika mtandaoni. Tembelea tovuti ya WCF kuomba usajili.
    Sajili WCF

  14. Hatua ya 14. Sajili Fire.

    Usajili wa Fire hufanyika ofisi zilizo karibu yenu. Mtalazimika kununua mitungi amba kufunga vifaa vingine vya kuzimia moto.
    Sajili Fire

  15. Hatua ya 15. Fungua account benki

    Tembelea tawi la benki inayowapendeza na ufungue account ya kampuni.
    Fungua Account Benki

Tools
  • 1. Computer yenye internet.
Materials
  • 1. Pesa kati ya TZS 750,000 na 3,400,000 kutegemea na aina ya kampuni na aina ya leseni.

Iwapo huna account kwenye mfumo wa BRELA ORS basi utapaswa kuunda account mpya kwanza ili uweze kuitumia kulogin na kujaza maombi. Bofya hapa kusoma jinsi ya kuunda account mpya kwenye mfumo wa BRELA ORS.

Ipo makala ihusuyo usajili wa kampuni BRELA kupitia mfumo wa usajili mtandaoni wa BRELA ORS. Makala hiyo unaweza kuipata kwa kubofya hapa.

Umependa makala hii kuhusu jinsi ya kusajili kampuni Tanzania? Je hungependa kupitwa na makala zetu? Tufuatilie Facebook, Twitter na Instagram. Una jambo la kuuliza? Karibu uwasiliane nasi kwa kobofya ama kubonyeza hapa.



Published by Kessy Juma

Kessy Juma

Kessy Juma is the founder of Miamia Trading Company (miamiatz). He is a Techpreneur with roots in accountancy. He believes that any business is good as long it caters the right market using the right strategy.

miamia miamia miamia miamia


Published by Kessy Juma

Kessy Juma Kessy Juma is the founder of Miamia Trading Company (miamiatz). He is a Techpreneur with roots in accountancy. He believes that any business is good as long it caters the right market using the right strategy.

miamia miamia miamia miamia
Was this page helpful?
YesNo
Scroll to Top