Biashara ya nafaka ya mtaji mdogo (Mchanganuo ulioboreshwa 2023)

Iwapo wewe ni muajiriwa na muda haukutoshi kujiingiza katika biashara kubwa zinazohitaji muda, basi amua kufanya biashara hii ya nafaka. Wapo ambao wanaishi katika nyumba zenye nafasi ya kutosha, pia wapo ambao wana chumba kimoja na sebule na hawana mahali pa kuhifadhi magunia kadhaa ya nafaka.

Ila iwapo una vyumba viwili basi angalia namna ya kugawa nafasi hiyo uweze kuweka hata angalau gunia 20 za kilo hamsini hamsini kwa kuanzia ili utapopata faida ya msimu huu uweze kujiwekea malengo ya kupangisha chumba kimoja cha ziada.

Kwa kawaida nafaka zote huwa bei ndogo wakati zinapovunwa na bei hupanda pole pole kadri muda unavyoenda. Hivyo hakuna siku utapata hasara kwa kuhifadhi nafaka zilizovunwa endapo utafuata taratibu za uhifadhi ili nafaka zisiharibiwe na wadudu ama panya.

Hebu tuchukulie kwa mfano, mwezi mmoja baada ya watu kuvuna mahindi na maharage ukaamua kununua kilo 500 za mahindi na kilo 500 za maharage. Ukazihifadhi katika magunia ya kilo hamsini hamsini. Utakuwa na gunia kumi za mahindi na gunia kumi za maharage.

Biashara ya nafaka – Manunuzi

Endapo utanunua mwezi wa mavuno kuna uwezekano mkubwa ukapata gunia la kilo mia za mahindi kwa 60,000/= na gunia la kilo mia la maharage kwa 200,000/=.

NafakaGuniaBei kwa guniaKiasi
Mahindi560,000300,000/=
Maharage5200,0001,000,000/=
Jumla101,300,000/=

Kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo juu, kilo 500 za mahindi itakuwa sawa na 300,000/= na kilo 500 za maharage itakuwa sawa na 1,000,000/=. Jumla ni 1,300,000/=.

Ukiona msimu wa mavuno umefika hebu wasiliana nao kule kijijini kila siku wakutumie japo kilo mia kwenye basi la abiria. Baada ya wiki mbili utakuwa ushapata hizo kilo 500 za mahindi na 500 za maharage.

Mauzo

Baada ya muda bei hupanda mpaka kufikia 100,000/= kwa gunia la mahindi na 300,000/= kwa gunia la maharage. Hapa ukiuza gunia tano za mahindi utapata 500,000/= na gunia tano za maharage utapata 1,500,000/=. Jumla 2,000,000/=

NafakaGuniaBei kwa guniaKiasi
Mahindi5100,000500,000/=
Maharage5300,0001,500,000/=
Jumla102,000,000/=

Kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo juu, kila gunia la mahindi ambalo ulilinunua kwa wastani wa 60,000/= sasa utaliuza kwa wastani wa 100,000/= hivyo utajipatia 500,000/= pesa ya mauzo ya mahindi pekee.

Vivyo hivyo, gunia la maharage ulilolinunua kwa 200,000/= msimu wa mavuno sasa utaliuza kwa wastani wa 300,000/= miezi kadhaa baada ya msimu wa mavuno ya maharage na kujipatia 1,500,000/= pesa ya mauzo ya maharage pekee.

Hii inamaana utajipatia jumla ya 2,000,000 kutoka kwenye hizo gunia 5 za maharage na 5 za mahindi. Usafiri na garama ya kuhifadhi gunia 10 inakadiriwa kuwa 200,000/=. Hivyo garama zako ni manunuzi 1,300,000/= jumlisha usafiri/uhifadhi 200,000/= jumla 1,500,000/=. Na faida yako ni 2,000,000 – 1,500,000 = 500,000/=.

Uhifadhi

Sasa hebu tuangalie namna ya kuhifadhi mahindi na maharage katika magunia. Kabla ya kuweka mahindi kwenye magunia inabidi kuchukua tahadhari ya kuzuia uharibifu utokanao na wadudu na panya.

Mahindi na maharage yanapaswa kuchanganywa na viua dudu. Viua dudu vinavyopendekezwa Tanzania ni Actelic Super Dust. Actelic Super Dust hupatikana maduka ya pembejeo. Kwa kawaida gramu 100 za kiuwadudu hiki huchanganywa na kilo 100 za mahindi/maharage.

Changamoto

Hakuna biashara isiyokuwa na changamoto. Kikubwa ni bora kuthubutu kuliko kubweteka. Mana anaejaribu mara kadhaa ana probability ya kufanikiwa kuliko asiejaribu kabisa.

Umeipenda makala hii? Usingependa kukosa makala kama hizi? Tufuatilie Facebook, Twitter na Instagram. Una jambo la kutujulisha? Tuambie kwa kubonyeza hapa.

Soma pia makala hizi hapa chini ili kunufaika zaidi: Biashara ya duka la reja reja, biashara za mtaji wa laki moja (100,000) kwa wafanya biashara wadogo

Imeandikwa na Kessy Juma

Kessy Juma ni muasisi wa Miamia Trading Company (MIAMIA). Ni Muhasibu aliyejikita zaidi kwenye biashara za kijiditali.
Was this page helpful?
YesNo
Scroll to Top