Jinsi ya kuanzisha duka la reja reja kwa mtaji wa Tshs laki tatu (Tshs 300,000)

Unaweza kuanzisha duka la reja reja kwa mtaji wa laki tatu ambapo utalazimika kukodi kibanda kwa ajili ya biashara hiyo. Soma makala kamili hapa.

Estimated Cost : 300000 TZS

Time Needed : 3 days

Jinsi ya kuanzisha duka la reja reja kwa mtaji wa Tshs laki tatu (Tshs 300,000).

  1. Hatua ya kwanza – Kukodi kibanda chako

    Tafuta kibanda cha kukodi cha Tshs 10,000 kwa mwezi na ulipe kodi ya miezi mitatu ambayo ni sawa na Tshs 30,000. Utabakiwa na Tshs 270,000. Hivi vibanda vinakodishwa sehemu kadhaa hasa hasa ukipita maeneo ya masoko ukaulizia wenye vibanda kama hivi watakuelekeza.Usijaribu kutengeneza chakwako mana unaweza maliza pesa yote kutengenezea kibanda kabla hata hujaanza kununua bidhaa. Hakikisha unatafuta cha kukodi.Kibanda-cha-biashara-duka la reja reja

  2. Hatua ya pili – Kukipeleka eneo husika

    Kukipakia kwenye mkokoteni na kukipeleka eneo husika itakugarimu wastani wa 10,000. Hakikisha hulipi zaidi ya hii. Kwa kawaida wabebaji ukizubaa wanakupiga pesa kubwa na ukikaza wanafanya nafuu.Kibanda-cha-biashara duka la reja reja

  3. Hatua ya tatu – Kukiandaa kibanda chako

    Tengenezamazingira ya kupanga vitu vyako ndani ya hicho kibanda cha duka la reja reja. Kwa kawaida vipo vitakavyohitaji kutundika, vipo vitavyohitaji kuning’iniza, vipo vitavyohitaji kuweka chini, vipo vitavyohitaji kutandikia chini kabisa. Hakikisha hutumii pesa kuandaa ndani ya kibanda chako.Kibanda-cha-biashara duka la reja reja

  4. Hatua ya nne – Kununua bidhaa za kuanzia

    Nunua bidhaa za msingi kabisa ambazo ni:Maji ya afya ya 500ml, 1ltr, 1.5ltr                               Tshs 40,000Vocha za Tshs 500 na Tshs 1,000                               Tshs 40,000Karanga za kufunga zilizokaangwa                          Tshs 5,000Ubuyu wa rangi uliofungwa kwa pakti                     Tshs 5,000Keki zile zilizotengenezwa kama maandazi             Tshs 5,000Jusi za chupa za plastiki                                                Tshs 20,000Mifuko hii ya kisasa iliyoruhusiwa                            Tshs 10,000Sabuni za kufunga na za vipakti                                 Tshs 30,000Chumvi za vipakti                                                          Tshs 10,000Viberiti vya kawaida na vya gesi                                 Tshs 5,000Dagaa wa kuopanga mafungu na wa pakti               Tshs 30,000Mayai ya kuchemsha                                                      Tshs 6,000Hapa utakuwa umeshatumia kama Tshs 216,000 unabakiwa na Tshs 54,000. Tumia hii kuongezea bidhaa mbali mabli kulingana na eneo husika.Kibanda-cha-biashara duka la reja reja

  5. Hatua ya tano – Kuanza biashara

    Baada ya kuweka bidhaa zote sasa ni wakati wa kufungua biashara yako. Kama unaweza pata benchi hata kama ni kutoka nyumbani kwako ama kwa rafiki basi weka kibenchi kinachoenea japo watu wawili mbele ya kibanda chako. Hakikisha unafungua mapema biashara yako na unachelewa kufunga usiku.Hii itasaidia watu wengi kujua kuwa wakija kwako hawawezi kukosa huduma hata kama ni usiku vipi. Uhakika wa huduma yako ni muhimu sana kwa baadhi ya wateja wanaoutumia zaidi usiku.Kibanda-cha-biashara duka la reja reja

  6. Hatua ya sita – Kutunza mahesabu

    Tunza mahesabu yako vyema. Ikifika jioni andika jumla ya mauzo ya siku na pesa ambazo umetoa kununua chochote kile kilichobidi. Kumbuka hupaswi kuielemea biashara kwa matumizi yako binafsi. Unapaswa kuwa bahili kwa kiasi kikubwa sana. Ukilega lega biashara inakuangukia.Kibanda-cha-biashara duka la reja reja

  7. Hatua ya saba – Kupanua biashara

    Jitahidi sana kila muda unavyoenda uongeze mtaji wako. Iwe ni kutokana na faida unayoitunza ama ni kuomba support kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki, na kadhalika. Kwa kawaida biashara za reja reja zinahitaji sana support ili kuimarika.Asante kwa kusoma mada hii ya kufungua duka la reja reja na kuendelea kufutilia mada za miamia. Tunashauri pia usome mada mbali mbali kwenye ukurasa wetu wa facebook (https://facebook.com/miamiatz)Kibanda-cha-biashara duka la reja reja

Tools
  • Kibanda
Materials
  • Matunda na mbogamboga

Published by Kessy Juma.

Kessy Juma is the founder of Miamia Trading Company (MIAMIA). He is a Techpreneur with roots in accountancy.
Was this page helpful?
YesNo
Scroll to Top