Unaweza kuanzisha duka la reja reja kwa mtaji wa laki tatu ambapo utalazimika kukodi kibanda kwa ajili ya biashara hiyo. Soma makala kamili hapa.
Estimated Cost : 300000 TZS
Time Needed : 3 days
Jinsi ya kuanzisha duka la reja reja kwa mtaji wa Tshs laki tatu (Tshs 300,000).
Hatua ya kwanza – Kukodi kibanda chako
Tafuta kibanda cha kukodi cha Tshs 10,000 kwa mwezi na ulipe kodi ya miezi mitatu ambayo ni sawa na Tshs 30,000. Utabakiwa na Tshs 270,000. Hivi vibanda vinakodishwa sehemu kadhaa hasa hasa ukipita maeneo ya masoko ukaulizia wenye vibanda kama hivi watakuelekeza.
Usijaribu kutengeneza chakwako mana unaweza maliza pesa yote kutengenezea kibanda kabla hata hujaanza kununua bidhaa. Hakikisha unatafuta cha kukodi.Hatua ya pili – Kukipeleka eneo husika
Kukipakia kwenye mkokoteni na kukipeleka eneo husika itakugarimu wastani wa 10,000. Hakikisha hulipi zaidi ya hii. Kwa kawaida wabebaji ukizubaa wanakupiga pesa kubwa na ukikaza wanafanya nafuu.
Hatua ya tatu – Kukiandaa kibanda chako
Tengenezamazingira ya kupanga vitu vyako ndani ya hicho kibanda cha duka la reja reja. Kwa kawaida vipo vitakavyohitaji kutundika, vipo vitavyohitaji kuning’iniza, vipo vitavyohitaji kuweka chini, vipo vitavyohitaji kutandikia chini kabisa. Hakikisha hutumii pesa kuandaa ndani ya kibanda chako.
Hatua ya nne – Kununua bidhaa za kuanzia
Nunua bidhaa za msingi kabisa ambazo ni:
Maji ya afya ya 500ml, 1ltr, 1.5ltr Tshs 40,000
Vocha za Tshs 500 na Tshs 1,000 Tshs 40,000
Karanga za kufunga zilizokaangwa Tshs 5,000
Ubuyu wa rangi uliofungwa kwa pakti Tshs 5,000
Keki zile zilizotengenezwa kama maandazi Tshs 5,000
Jusi za chupa za plastiki Tshs 20,000
Mifuko hii ya kisasa iliyoruhusiwa Tshs 10,000
Sabuni za kufunga na za vipakti Tshs 30,000
Chumvi za vipakti Tshs 10,000
Viberiti vya kawaida na vya gesi Tshs 5,000
Dagaa wa kuopanga mafungu na wa pakti Tshs 30,000
Mayai ya kuchemsha Tshs 6,000
Hapa utakuwa umeshatumia kama Tshs 216,000 unabakiwa na Tshs 54,000. Tumia hii kuongezea bidhaa mbali mabli kulingana na eneo husika.Hatua ya tano – Kuanza biashara
Baada ya kuweka bidhaa zote sasa ni wakati wa kufungua biashara yako. Kama unaweza pata benchi hata kama ni kutoka nyumbani kwako ama kwa rafiki basi weka kibenchi kinachoenea japo watu wawili mbele ya kibanda chako. Hakikisha unafungua mapema biashara yako na unachelewa kufunga usiku.
Hii itasaidia watu wengi kujua kuwa wakija kwako hawawezi kukosa huduma hata kama ni usiku vipi. Uhakika wa huduma yako ni muhimu sana kwa baadhi ya wateja wanaoutumia zaidi usiku.Hatua ya sita – Kutunza mahesabu
Tunza mahesabu yako vyema. Ikifika jioni andika jumla ya mauzo ya siku na pesa ambazo umetoa kununua chochote kile kilichobidi. Kumbuka hupaswi kuielemea biashara kwa matumizi yako binafsi. Unapaswa kuwa bahili kwa kiasi kikubwa sana. Ukilega lega biashara inakuangukia.
Hatua ya saba – Kupanua biashara
Jitahidi sana kila muda unavyoenda uongeze mtaji wako. Iwe ni kutokana na faida unayoitunza ama ni kuomba support kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki, na kadhalika. Kwa kawaida biashara za reja reja zinahitaji sana support ili kuimarika.
Asante kwa kusoma mada hii ya kufungua duka la reja reja na kuendelea kufutilia mada za miamia. Tunashauri pia usome mada mbali mbali kwenye ukurasa wetu wa facebook (https://facebook.com/miamiatz)
Tools
- Kibanda
Materials
- Matunda na mbogamboga
Published by Kessy Juma.
Kessy Juma is the founder of Miamia Trading Company (MIAMIA). He is a Techpreneur with roots in accountancy. |